Friday, August 17, 2012

KAMANYOLA MARQUIS!

:Nguza Viking,Banza Mchafu(RIP),Mulenga Kalonji(RIP),King Kiki,Kabeya Badu,Nkulu Wabangoie,Mbuya Makonga(RIP),Tshibangu Katay(RIP),Tshinyama Tshiyanza(RIP),Kanku Kelly,Mzee Tito(RIP),Ilunga Bizzos(RIP),Parash Mukumbule,Kiniki Kieto,Mwema Mujanga,Kimeza Abdallah(RIP).

Pia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....

Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpen zi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwati pwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwac ha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....


Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............


Hakika ya kale ni dhahabu...

No comments:

Post a Comment